Q amedai kuwa wimbo ni kwaajili ya kuondoa ‘chawa’ wa mjini.
“Kuna ngoma mpya inaitwa Chawa,” muimbaji huyo alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Unajua mjini kuna Chawa wengi kuna jinsi ya kuwapunguza. Chawa ni kama neno linalokuja ku-take over, kwa sababu mimi ni mtu wa misemo hata historia ya nyimbo zangu nyingi ambayo inabaki. Najua mjini kuna Chawa wengi na ni kisa cha kweli. Najua huu wimbo utaniletea matatizo mengi lakini mimi lakini mwisho wa siku sijali ndio kazi ya muziki, siwezi kusema kuna watu nimewalenga ila nimezungumzia ukweli. Namshukuru mungu management yangu wananiunga mkono kwahiyo mjini Chawa inabidi wapungue.”
Amesema wimbo huo umetayarishwa na Man Walter wa Combination Sounds.
0 comments:
Post a Comment