Rais MUGABE karudi kwenye headlines baada ya maamuzi haya kutoka kwa wapinzani…

Mwezi uliopita Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya wabunge wa vyama vya upinzani kumzomea wakati akitoa hutuba wakimshutumu kushindwa kuiongoza vyema nchi yao.
Headlines zimerudi tena kwa Rais huyo baada ya jana Bunge hilo kuahirisha matangazo ya LIVE ya redio na Televisheni ya hotuba ya Mugabe kutoka kwa vyama vya upinzania kutishia kuvuruga hotuba hiyo kwa mara nyingine.
Wapinzania hao wamekua wakimlaumu rais wao kuendelea kung’ang’ania madarakani wakati uchumi wa nchi hiyo ukiendelea kudidimia kila siku.
Rais Mugabe ambaye sasa ametimiza miaka 91 amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.
Spika wa Bunge Jacob Mudenda amevionya vyama hivyo kuacha mara moja vurugu hizo lakini ziligonga mwamba na vituo vya matangazo kusitisha kurusha matangazo hayo LIVE.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment