Ray Awapa Makavu UKAWA






Vincent Kigosi ‘Ray’ 

Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameendelea kushusha maneno kwa chama kinachounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya kufunguka hadharani kuwa hawakuwa na sera ambazo zingemfanya aendelee kubaki.

Staa huyo ambaye kwa sasa amerudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kurudi kwake CCM hakumaanishi kama amehongwa kama watu wanavyoendelea kusambaza habari hizo bali amekwenda kutokana na kuvutiwa na sera.

“Naomba nieleweke kuwa dhamira yangu ya kubaki Ukawa ndiyo ilikuwa ikinisuta. Nikiwa kama mmoja wa wasanii, nimevutiwa na sera za CCM hasa kwa upande wa wasanii ambapo Mgombea Urais, Magufuli (John Pombe) alisema moja ya sera zao ni kujali maslahi kwa wasanii na kuwafungulia mfuko maalum utakaowashughulikia,” alisema Ray.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment