Tunda Man anatarajia kuachia wimbo mpya ‘Mama Kija’ utakaoelezea jinsi alivyomtesa mama yake wakati wa ujauzito.
Tunda ameiambia E-Newz ya EATV kuwa ameamua kuandika wimbo huo ili kuonyesha jinsi gani mama yake alivyoteseka kwaajili yake.
“Napata hongera nyingi kutoka kwa watu wangu kwa sababu wanahisi mke wangu ni mjamzito,” alisema msanii huyo.
“Lakini kitu ambacho nataka kuwaambia watanzania kwamba ‘Mama Kija’ ni wimbo wangu mpya. Ni wimbo ambao unaelezea jinsi mimba yangu ilivyokuwa inasumbua. Mama yangu alinihadithia ni jinsi gani alivyokuwa anamsumbua baba yangu kwa sababu ya mimba yangu. Kwahiyo vitu ambavyo alikuwa ananihadithia ndio nikatunga wimbo. Mama yangu baada ya kusikia huo wimbo chozi lilimtoka,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment