UKILAZA Wambikiza Shule Mwigizaji Riyama..Ashindwa Kumaliza Shule Kisa Ugumu wa Maisha




Riyama Ally
KILAZA! Staa wa Filamu Bongo, Riyama Ally ameweka wazi kuwa hakumaliza elimu ya sekondari kutokana na ugumu wa masomo kwani hakuwa akiambulia chochote darasani licha ya walimu kujitahidi kufundisha kwa kiwango cha juu.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Riyama alisema kuwa kutokana na umbumbumbu wake alilazimika kuishia kidato cha pili baada ya masomo kuzidi kuwa magumu.

“Kwa kweli ugumu wa masomo ulinifanya niache shule, niliona kama wazazi wanapoteza pesa yao bure, sikuwa naambulia chochote, walimu walikuwa wakijitahidi sana lakini sikuwa naelewa kitu, kwa hiyo nimekomea kidato cha pili, masomo magumu asikuambie mtu,” alisema Riyama.

Source:Global Publishers
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment