Video: Hemedy ana ushauri kwa wanaume wa jinsi ya kumfanya mpenzi wako asikuache kamwe!

Hemedy PHD amejifunza kuwa kutulia na mpenzi mmoja, kuwa mwaminifu, kumpa muda wako mwingi haitoshi kumfanya mwanamke awe na furaha.



Akiongea na Round Up, Hemedy amesema amegundua kuwa kuna vitu vingine vinavyoonekana kuwa ni vidogo lakini ni sumu katika uhusiano.

“Ni tabia ndogo ndogo za wivu, ukorofi, ni vitu ambavyo mimi nilikuwa navyo ambavyo nilikuwa nafikiria kuwa hivi haviwezekani mimi nikaachwa, kwasababu sijacheat, sijampiga,” amesema Hemedy.

“Nilikuwa nafanya vitu vingine, ‘uko wapo, ofisini, mpaka sasa hivi hujatoka, matusi sometimes, wivu na vitu vingine.”
Amesema wakati mwingine alikuwa anamnyima uhuru mpenzi wake na hivyo kujikuta akim-boa kwa kiasi kikubwa kitu ambacho hata mama yake alimuonya.
Hemedy amesema vitu hivyo ndivyo vilimfanya aachane na mpenzi wake na kutunga wimbo ‘Imebaki Story’ japo wamerudiana tena baada ya kujirekebisha.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment