Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV jana, Kalama alisema aliona asingeweza kufanya vizuri bila kuwa na management.
“Sasa hivi nimerudi kweli kwa sababu muda ambao nimekaa kimya nilikuwa sina management. Unajua hata mtoni akina Nas wanakuwa na management that’s why wanakuwa wanafanya vitu ambavyo vinaeleweka,” alisema.
“Kwahiyo mimi nikaona kwanza nipumzike nikipata management nirudi. Kwahiyo sasa hivi nina management. Nimepata mshikaji wangu Gelly ndio atasimamia kila kitu. Huyu ndio meneja wangu. Kwahiyo sasa hivi ni kitu baada ya kitu. Baada ya miezi miwili kitu.”
0 comments:
Post a Comment