Mke wa Master P, Sonya Miller anamshtaki mwanae wa kiume, Romeo, kwa mujibu wa TMZ.
Familia ya Master P
Sonya anadai kuwa Master P amekuwa akimtumia Romeo kuficha mali zake wakati wa masuala ya talaka yao yakiendelea. Amedai kuwa kampuni ya No Limit Forever iliyokuwa No Limit Records awali ni mfano wa ujanja wa mumewe.
Romeo ametajwa kama mwanzilishi na mmiliki wa kampuni hiyo iliyoanza mwaka 2010. Sonya alikuwa akisimamia No Limit Records na mume wake tangia miaka ya 1990 na anadai kuwa No Limit Forever ni mpango wa kumzuia kwenye lebo hiyo.
Anadai pia mume wake kupitia kipindi cha reality cha Master P’s Family Empire ameweka kibindoni kiasi cha $750,000 kwA kumweka Romeo kwenye orodha ya wanaolipwa.
Miller alitaka apewe talaka na Master P mwaka 2013.
0 comments:
Post a Comment