Afungua mashtaka ya filamu ya mauaji ya John F Kennedy



Image captionGari aina ya Limousine la rais John F Kennedy

Mwanamke mmoja ambaye babu yake alichukua ukanda wa video wa mauaji ya rais John F Kennedy kama filamu ya nyumbani ameishtaki serikali ya Marekani kwa mapato yake.

Gayle Nix Jackson pia anataka kulipwa fidia ya dola milioni 10 za filamu hiyo iliochukuliwa na Orville Nix mnamo mwezi Novemba mwaka 1963.

Aliiuza filamu hiyo kwa shirika moja la habari mwaka huo lakini baadaye ilipewa serikali ili uchunguzi ufanywe.

Bi Nix Jackson anasema kuwa aliambiwa mwaka huu kwamba shirika hilo la habari la serikali linalodaiwa kumiliki kanda hiyo halina.

Kanda hiyo ilichukuliwa na filamu ya Nix mkabala na upande ambapo gari la rais aina ya Limousine lilikuwa, kutoka mahala ambapo filamu maarufu ya Zapruder ilichukuliwa tarehe 22 mwezi Novemba 1963.

Filamu hiyo ya Nix inaonyesha risasi ikimpiga rais,mkewe rais Jackie Kennedy akipanda juu ya gari hilo na jasusi Clint Hill akiruka na kuingia ndani ya gari hilo.

Orville Nix aliiuza filamu yake kwa UPI kwa dola 5,000 kukiwa na makubaliano ya malipo mengine baada ya miaka 25.

Lakini baadaye ilipewa serikali ili uchunguzi ufanywe.

Ilionekana mara ya mwisho na kamati ya bunge iliokuwa ikichunguza mauaji hayo mwaka 1978.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment