Bila Lollypop nisingekuwa hapa nilipo leo – Mo Music
Muimbaji wa ‘Basi Nenda’ Moshi Katemi maarufu kama Mo Music, amesema kuwa bila kufanya kazi na mtayarishaji na mwandishi wa nyimbo Lollypop huenda angechukua muda mrefu sana kufikia mafanikio aliyonayo sasa.
Lollypop ndiye mwandishi wa ‘Basi Nenda’, wimbo uliomtambulisha na kumfungulia njia Mo Music kwenye game ya Bongo fleva.
“Lolly Pop anajua uwezo wangu wa uimbaji ukoje na ananisapoti sana, bila Lolly pop nafikiri MO Music angechelewa sana kuanzia kwenye basi nenda mpaka sasa hivi, ushirikiano wake ni 90%”, Alisema Mo Music kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.
Akizungumzia wimbo wake mpya ‘Skendo’, Mo amesema anautabiria kufanya vizuri sana.
“Skendo naitabiria kuwa mega hit, nafikiri imevunja rekodi ya nyimbo zangu zote ndani ya masaa manne kwa sababu mimi huwa natathimini nyimbo zangu ndani ya masaa manne tangu niiachie” alieleza Mo Music jkutoka Mwanza.
0 comments:
Post a Comment