Hakuna usawa wa upigwaji nyimbo za wasanii redioni – Msechu
Peter Msechu amelalamikia ukiritimba uliopo katika vyombo vya habari na kudai ndio unaosababisha nyimbo nzuri kutopata nafasi za kufanya vizuri.
Akizungumza katika kipindi The Jump off cha Times FM, Msechu alisema amekuwa akijaribu mara kwa mara kufanya ‘ngoma’ nzuri kwa maendeleo ya Bongo Flava lakini huwa hazieleweki zinapoishia.
“Nafikiri kuwe na utaratibu mzuri redioni, kuwe na usawa katika upigaji nyimbo,” alisema. “Sasa kama mmoja atalia mara moja halafu mwingine mara kumi tutakuwa tunafelishana tu. Ifike kipindi tupewe nafasi sawa halafu kizuri kijiuze wananchi wenyewe waamue. Kuna mambo lazima tuyaache.”
0 comments:
Post a Comment