Rose Ndauka ajibu tetesi za kuwa na uhusiano na Shetta



Baada ya kuenea tetesi kuwa mke wa Shetta ‘Neila Yusuf’ anadai talaka kwa mume wake kutokana na Rose Ndauka kuingilia ndoa yao, Ndauka amevunja ukimya.



Akiongea kwenye kipindi cha Mkasi, Ndauka alikanusha kuwahi kuwa na uhusiano na rapper huyo.

“Kuna siku nilikuwa kwa Diamond, Mama Kayla alikuwepo, kwahiyo akawa amenifuata kunisalimia, Dareen akawa ananiambia umemuona ‘mama Kayla?’ Nikamwambia yupo wapi? akaniambia ndio huyu hapa! Nikawa nacheka nikamwambia ‘mambo’, nikamwambia nasikia umeondoka kwako kwaajili yangu? Akaanza kucheka, akaniambia ‘sio kweli mbona hakuna kitu kama hicho.’ Kwahiyo nikacheka kwa sababu mtu mwingine anaweza kucreate tu kitu kwa sababu tu hawajamuona Rose kwenye magazeti. So wanataka kumweka kwenye zile skendo ili awe mmoja kati ya wasanii wenye skendo,” alisema Ndauka.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment