Chris Brown abadili tarehe ya kuachia album yake ‘Royalty’ iliyokuwa itoke Ijumaa hii

Yale yaliyojitokeza kwenye album iliyopita ya Chris Brown, ‘X’ (kuahirisha tarehe ya kuachia) yameanza kujitokeza tena kwenye album yake mpya ‘Royalty’ ambayo hapo awali ilipagwa itoke Ijumaa hii November 27 lakini sasa imesogezwa mbele.



Chris Brown mwenyewe amethibitisha kuwa sasa album yake hiyo itatoka December 18 mwaka huu.

Hadi jana Nov 23. Breezy alikuwa akipromote tarehe 27 kuwa ndio angeachia ‘Royalty’, lakini taarifa za terehe mpya amezitoa kupitia mahojiano mapya aliyofanya na Nessa wa Hot 97.

Chris amesema Nov.27 ambayo ndio ingebidi album itoke, itakuwa tarehe kwa wale watakaopenda kuweka ‘pre-order’, pia ataitumia siku hiyo kutoa orodha ya nyimbo zitakazokuwemo kwenye album pamoja na snippets.

Royalty itakuwa ni album ya saba ya Chris Brown. Zilizopita ni ‘Chris Brown’ (2005), ‘Exclusive’ (2007), ‘Graffiti’ (2009), ‘F.A.M.E.’ (2011), ‘Fortune’ (2012) pamoja an ‘X’ (2014). Pia yeye na Tyga walitoa album ya ushirikiano ‘Fan of a Fan: The Album’ (2015).

Msililize Breezy akitaja tarehe mpya

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment