Shaa kuachia video iliyoongozwa na Justin Campos ‘soon’


Hivi karibuni wasanii wamekuwa na tabia ya kushoot video kali na kukaa nazo ndani bila kusema chochote.



Shaa ni mmoja wapo. Ukimya wake haumaanishi kuwa hakuna vitu vikubwa vinavyofanyika nyuma ya pazia. Muimbaji huyo miezi kadhaa iliyopita alisafiri hadi Afrika Kusini kwenda kushoot video ya wimbo wake na muongozaji aliyejikusanyia sifa Afrika, Justin Campos.

Mke wa Justin, Candice, amepost picha ya screeshot kwenye Instagram kutoka kwenye kile kinachoonekana ni video ya wimbo huo uitwao Toba na kuandika: Something Awesome coming!!! @shaa_tz @masterjtz.”






Kwenye picha hiyo Shaa anaonekana akiwa amejichora hina ya kutosha.

Yeye mwenyewe ameweka picha mbalimbali kama hizo kwenye Instagram bila kuandika chochote.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment