Kuna kipindi Nay Wa Mitego alitangaza kuwa ana mpango wa kuanza kujitambulisha kwenye soko la kimataifa
, kwa kufanya collabo na wasanii wa nje pamoja na kushoot video nje ya Tanzania pia.
Katika mahojiano ya siku za nyuma na Bongo5, Nay alisema tayari amekamilisha collabo na msanii wa Nigeria, Runtown, na alikuwa kwenye mipango ya kutafuta uwezekano wa kufanya kazi na Wizkid an D’Banj.
Wiki hii Nay Wa Mitego ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Nyumbani Kwetu’, hata kama hujausikia sina haja ya kuwambia kama ni wa kimataifa ama laa, kwasababu hata jina tu linajieleza.
Muimbaji huyo wa ‘Muziki Gani’ amesema alibadili mawazo ya kuitoa collabo yake na Runtown kipindi hiki.
“Plan ilikuwa itoke kabla ya ‘Sina Muda’, lakini kila kitu kinaenda kwa mipango pia lazima uangalie timing, halafu muziki ni biashara, sitaki nifanye kwaajili ya kuwaridhisha tu watu kwamba na mimi nimefanya, nataka nikifanya basi dunia ijue kuna msanii mpya amekuja kwenye dunia nyingine.” Nay ameiambia Bongo5.
Nay aliendelea,
“Imefika time nikapeleka hii mipango mbele nikasema mwaka huu acha nimalizane na watu wa nyumbani kwanza, ndio maana ukaona ikatoka ‘Sina Muda’ nilikuwa nadaiwa wimbo wa kurap, pia wimbo niliacha sasa hivi ‘Nyumbani Kwetu’ ni wimbo wa tofauti sijawahi kufanya muziki wa namna hii, yote ni katika kuwasurprise watu wangu wa nyumbani, lakini nataka nikianza kupiga hatua nyingine kuondoka nyumbani na kwenda sehemu nyingine basi iwe nimesema sasa nimeamua kuanza safari rasmi.”
True Boy amemaliza kwa kwa kusema kuwa anatarajia kuutoa wimbo alionshirikisha Runtown mwakani, na ndio utakuwa mwanzo wa safari yake kwenda kimataifa.

0 comments:
Post a Comment