Filamu ya Tanzania ‘Dogo Masai’ yaibuka kidedea tuzo za Marekani
Wakati ambapo kiwanda cha filamu Tanzania kinaendelea kudoda, kuna habari njema kutoka wa filamu ya ‘Dogo Masai.’ Filamu hiyo ya Kitanzania imeshinda tuzo tatu.
Hii ni taarifa zaidi:
Ninaitwa Timoth Conrad Kachumia Director, Producer na Writer wa filamu Tanzania. Ninayofuraha kuwajulisha watanzania kuwa nimefanikiwa kushinda California Viewers Choice Awards 2015, tuzo 2 ikiwa ni Best Feature Film pamoja na Best Director kupitia filamu ya DOGO MASAI, vile vile kutoka katika filamu hiyo hiyo Omary Clayton ambaye ni muigizaji mkuu amefanikiwa kushinda tuzo ya Best Actor.
Filamu ya Dogo Masai ni filamu ambayo inamzungumzia kijana mdogo ambaye anapitia wakati mgumu baada ya kudhulumiwa mali zake na Mjomba wake, hivyo anajikuta akiuvaa uhusika wa kimasai kutokana na kutupwa porini na kuokotwa na wamasai. Dogo Masai ni jina alilolitumia wakati wote kwenye filamu.
Upatikanaji wa washindi ulifanyika kupitia kura za mitandaoni na watu mbali mbali walionyesha kusapoti sana kwenye hatua ya kupiga kura na hatimaye kutuwezesha kushinda tuzo hizo ambazo ni za heshima kwa sababu zinatokana na majibu ya watazamaji wa filamu. Filamu zote za washiriki zilionyeshwa online kwenye mtandao wa www.cvcawards.com na kupigiwa kura. Hivyo kura zimekusanywa kutoka kwa watazamaji wa kwenye mtandao.
0 comments:
Post a Comment