‘Don’t Bother’ imetimiza moja ya ndoto alizokuwa nazo rapa wa Weusi, Joh Makini za kuja kufanya collabo na rapa wa Afrika Kusini Kiernan Jarryd Forbes a.k.a AKA.
Joh Makini amewataja ma-rapper aliokuwa, na ambao bado anatamani kuja kufanya nao collabo pindi fursa hiyo itakapojitokeza, akiwemo AKA ambaye tayari amefanikiwa kufanya naye ‘Don’t Bother’ inayofanya vizuri kwa sasa.
“Unajuaga kunakuwaga na watu wako flani ambao unawaskilizaga pia na unapenda wanachokifanya kwamba siku ikitokea unapata nafasi ya kukutana nao ungependa kufanya nao kitu.” Joh Makini alisema kupitia Planet Bongo ya EA Radio. “Kwanza (AKA) ni mmoja kati ya wasanii wakubwa sana kwa saivi barani Afrika na kidunia kwa ujumla, ni msanii wa Hip Hop ambaye msanii yeyote wa Hip Hop wa nchi nyingine anapokutana naye angetamani kufanya naye ngoma . Actually ni moja ya rappers ambao wako kwenye list yangu ambayo nilikuwa nimepanga kwamba endapo nitakuja kukutana na KO ama AKA au Sarkodie siku moja au M.I.” alimaliza Joh.
‘Don’t Bother’ ndio wimbo ulioongoza kwa kuchezwa zaidi kwenye vituo vya radio na TV Tanzania kwa wiki ya kuanzia Nov.23 hadi Nov.29 kwa mujibu wa CMEA Tanzania.
0 comments:
Post a Comment