Lollipop ashinda tuzo ya ‘Wimbo wa Mwaka’ kwenye Xtreem Awards za Kenya
Muimbaji, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa muziki, Goodluck Gozbert maarufu kama Lollipop ameanza kuonja mafanikio ya kipaji chake kwa kushinda tuzo ya kwanza, Xtreem Awards 2015 zilizotolewa Nairobi, Kenya Jumapili Dec.20.
Goodluck ameshinda kipengele cha ‘Tanzanian Artist/Song of the Year’ ambapo alikuwa akishindana na waimbaji wengine wa muziki wa injili wakiwemo Bonny Mwaitege, Edson Mwasabwite, Enock Jonas, Christopher Mwahangila na wengine.
Mtayarishaji huyo wa hit songs za Barakah Da Prince ‘Siachani Nawe’ na ‘Nivumilie’, pamoja na ‘Basi Nenda’ ya Mo Music amezungumza na Bongo5 kuelezea tuzo aliyoshinda inamaana gani kwake.
Muwakilishi wa Goodluck akimpokelea tuzo yake Kenya
“Hii tuzo imefanyika kuwa hatua kubwa sana kwenye muziki wangu, motisha kwa malengo yangu lakini pia imefanyika kuwa kumbukumbu katika maisha ma muziki wangu kwa ujumla hasa ukizingatia kuwa ndio tuzo ya kwanza kabisa kwangu lakini pia tuzo toka nje ya mipaka ya tanzania. Nimefarijika sana, na kwangu moja ya hatua kubwa ambayo sitosahau na kuiheshimu,” amesema Goodluck aka Lollipop.
Alimaliza kwa kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura iliyompa ushindi wa tuzo hiyo.
“Napenda kuwashkuru, Watanzania wote na mashabiki wa muziki wangu nje na ndani ya tanzania kwa kunipigia kura lakini pia vyombo vyote vya habari, wadau wa muziki mbali mbali na watu binafsi waliojitolea kwa namna moja au nyingiine kunifikisha hatua hii, nawashkuru sana.” alimaliza Goodluck.
0 comments:
Post a Comment