Lord Eyez aupania mwaka 2016



Rapa kutoka Weusi, Lord Eyez ameonesha kuupania mwaka 2016, kuufanya uwe ni mwaka wa kulipa madeni yote anayodaiwa na mashabiki wake waliomkosa kwa kipindi kirefu.


Ukimya wake uliosababisha kuwepo na maswali mengi likiwemo la kama ametengana na Weusi ulivunjwa na rapa huyo hivi karibuni alipoweka wazi kuwa bado yupo Weusi.

“Napenda kuwaambia mashabiki zangu kuwa mwaka 2016 ni mwaka wangu sasa kufanya kweli, kwani ukimya wangu umeendana na kupika kazi mpya na mpaka sasa nimeshafanya kazi mbili na G Nako vitu vinakuja kwenye masikio yao wakae mkao wa kula.” Alisema Lord Eyez kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Hapo awali Weusi walimsimamisha rapa huyo kutokana na matatizo yaliyojitokeza miezi kadhaa nyuma ya rapa huyo kuhusishwa na matukio ya wizi, lakini baadae walimsamehe.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment