Magufuli aivunja bodi ya bandari, TPA


Rais Dkt John Magufuli ameivunja bodi ya mamlaka ya bandari, TPA.



Uamuzi huo umetangazwa Jumatatu hii na waziri mkuu, Kassim Majaliwa.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Majaliwa amesema Dkt Magufuli ametengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi ya bandari, Profesa Joseph Msambichaka na Mkurugenzi wa bandari, Awadh Massawe.

Pamoja na hivyo rais pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa wizara ya uchukuzi, Dkt Shaban Mwinjaka atakayepangiwa kazi nyingine.

Hatua hiyo imekuja baada ya waziri mkuu kufanya ziara mbili za kushtukiza bandarini na kubaini uwepo wa vitendo vya rushwa uliokithiri pamoja na ukwepaji mkubwa wa kodi.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment