Manchester United yatolewa nje UEFA


Manchester United jana Disemba 8 imeiaga rasmi michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kupata kipigo cha magoli 3-2 na Wolfsburg ya Ujerumani kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B uliokuwa unaamua timu gani zitasonga mbele kwenye hatua ya mtoano kati ya timu tatu zilizokuwa na nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua hiyo.



United, Wolfsburg na PSV zote zilikuwa na nafasi ya kufuzu kwenda kwenye hatua ya 16 bora lakini United imejikuta ikishindwa kusonga mbele.



Anthony Martial alianza kuifungia goli Manchester United dakika ya 10 lakini bao hilo halikudumu baada ya dakika tatu kusawazishwa na Naldo. Vieirinha akaipatia Wolfsburg bao la pili dakika ya 29 na kufanya matokeo kuwa 2-1 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.



Dakika ya 82 Wolfsburg walijifunga kupitia mchezaji wao Guilavogui na kuipa matumaini Man United huenda ingepata nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo lakini dakika ya 84 Naldo alizima matumani yao.

Kama United ingetoka sare kwenye mchezo huo, ingekuwa bado safari yao ya kuyaaga mashindano hayo haikwepeki kutokana na ushindi wa magoli 2-1 iliyoupata timu ya PSV dhidi ya CSKA Moscow.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kujikuta imeangukia kwenye ligi ya EUROPA (UEFA ndogo).

Haya ni matokeo ya mechi zingine zilizochezwa Jumanne usiku:

Paris St Germain 2 – 0 Shakhtar Donetsk
Real Madrid 8 – 0 Malmö FF
VfL Wolfsburg 3 – 2 Man Utd
Manchester City 4 – 2 B Monchengladbach
PSV Eindhoven 2 – 1 CSKA Moscow
Benfica 1 – 2 Atl Madrid
Galatasaray 1 – 1 FC Astana
Sevilla 1 – 0 Juventus


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment