Watakaocheza pool saa za kazi kukiona





Mkuu wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Crispian Meela amepiga marufuku mchezo wa pool saa za kazi na kuonya atakayekiuka agizo hilo, atamchukulia hatua kali za kisheria.


Meela alitoa amri hiyo juzi wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri za mji wa Babati na Wilaya ya Babati.


Alisema amebaini kuwa watu wengi wilayani hapa wanatumia muda mwingi wa kazi kucheza mchezo huo badala ya kufanya shughuli za maendeleo.


Meela alisema vijana wengi ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa hujazana kwenye baa kuanzia asubuhi wakicheza pool badala ya kujishughulisha na kazi za uzalishaji mali.


“Kuanzia Desemba Mosi (leo) mwaka huu, mchezo huo utaanza kuchezwa saa 10 jioni siku za kazi na kuanzia saa 8 mchana siku za mwisho mwa wiki,” aliamuru Meela.


Alisema ametoa amri hiyo kwa wakazi wote wa wilaya hiyo wanaoishi mjini na vijijini.
Alisema hivi karibuni alifanya ziara kwenye kijiji kimoja wilayani hapa na kushuhudia baadhi ya vijana wakicheza pool saa za kazi.


Baadhi ya wamiliki wa mchezo huo walilamikia amri hiyo wakisema itawaathiri kwa kukosa kipato kutokana na mchezo huo. “Mimi hucheza mchezo mmoja kwa Sh200, muda wa kucheza ukipunguzwa nitakuwa naingiza kipato kidogo kwa siku tofauti na sasa, ” alisema Omary Juma, mkazi wa Maisaka
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment