Chege adai ana mkasirisha mama yake kutoswali swala tano
Msani wa muziki kutoka Kundi la TMK Wanaume Family, Chege Chigunda amesema ingawa Mama yake amemruhusu kufanya muziki lakini bado ana deni la kuswali swala tano kama agizo la mama yake.
Chege ambaye anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Sweety Sweety’ amekiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa Mama yake ni mtu wa swala tano kabisa.
“Kitu ambacho naweza sema kinachomkasirisha Mama yangu ni kutoswali swala tano,” alisema.
“Unajua Mama yangu ni mtu wa swala tano sana. Sasa mimi nimetokea kufanya vitu tofauti kabisa ambavyo haviendani nae lakini ameamua kuvikubali kwa sababu anaona navifanya kwa njia nyoofu. Sivifanyi alafu nikawa doa kwake, sijamtia aibu,” alisema Chege.
0 comments:
Post a Comment