Director Nisher kurudi kwa kishindo, aahidi kuachia video tatu kwa mpigo mwezi huu


Nisher is back! Mshindi wa tuzo ya Muongozaji wa Video Anayependwa katika Tuzo Za Watu 2014, director Nisher ameanza ku-tease ‘come back’ yake baada ya ukimya mrefu.

Nisher

Nisher ambaye mwaka jana (2015) alipiga story na Bongo5  na kueleza changamoto mbali mbali zilizomsababisha kuamua kukaa pembeni kwa muda, ameanza kuwaweka tayari mashabiki wa muziki wajiandae kupokea video tatu mpya kwa mpigo kabla mwezi Februari haujaisha.

“Natamani muone mambo nliyowaandilia… Spendi kuongea sana skuizi, maneno mengi sio Dili… kabla mwezi hauja isha Nawashushia Video Tatu za nguvu Kwa Mpigo!! #GETREADY #NIMEKASIRIKASANA #NISHERISBACK #Three_in_One” ameandika Nisher Instagram.

Nisher ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kufanya ‘comeback’ ya tofauti kwa kuachia video tatu kwa mpigo japo mwanzo alipanga ziwe video saba kwa mara moja, zikiwa ni za wasanii tofauti.
“Niliona nikitoa moja moja Itakua common sana na mi huwa sipendi kufanana au kufananishwa so mpango wa kwanza nlitaka nitoe video 7 kwa mpigo lakini nikaona kama nitasumbua sana acha nianze na 3 kwanza” alisema Nisher.
“Video hizi zitakua na ladha ya tofauti Kila moja na ukubwa tofauti so Kila mtu ataridhika kwa maramoja, tofauti na ningetoa moja moja” aliongeza Nisher.
Hata hivyo Nisher hajapenda kutaja majina ya wasanii ambao video zao zinaanza kutoka mwezi huu, lakini amesema moja itakuwa ni ya Weusi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment