Kim Kardashian adaiwa kukerwa na tabia ya Kanye West ya kulalamika kwenye Twitter


Kim Kardashian hataki mume wake Kanye West aendelee kumwaga malalamiko kibao kwenye Twitter.



Pamoja na kwamba amekuwa akimuunga mkono mume wake kwenye mambo mengi, jarida la People limedai kuwa hapendi kuona akiendelea kuitumia Twitter vibaya.Chanzo kimeliambia jarida hilo kuwa tweets hizo za Kanye zimeendelea kusababisha malumbano kwenye ndoa yao.

Katika kipindi cha hivi karibuni Kanye amekuwa akitweet drama nyingi zinazosababisha awepo kwenye headlines kila siku.

Hivi karibuni alidai kuwa ana deni la dola milioni 53 na alimuomba mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg dola bilioni 1 kusaidia kufanikisha ndoto zake.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment