Nisher afafanisha ujio wake mpya kama wa Nicolas Cage kwenye Ghost Rider



Moto utawaka, minyororo yenye moto itarushwa na pikipiki zenye speed zitaunguruma!



Huo ni ujio mpya wa muongozaji wa video za muziki nchini, Nisher ambaye mwaka wote wa 2015 alikuwa kimya.



Kuonesha kuwa mwaka 2016 utakuwa wa kazi tu, muongozaji huyo wa Arusha amepost picha ya cover ya filamu ya Nicolas Cage, Ghost Rider kutia msisitizo wa jinsi mwaka huu utakavyokuwa wa moto.

Hata hivyo tofauti na Cage, silaha yake kubwa ni kamera.

Miongoni mwa wasanii wa kwanza atakaofanya nao kazi mwaka huu ni G-Nako na msanii chipukizi, The Voice Fairy.

Tunasubiri kuona alichonacho mwaka huu.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment