Producer na CEO wa Bhitz Music Group, Hermy B amewataja wasanii anaotamani kufanya nao kazi, akiwemo Diamond.
Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatatu hii, Hermy B alisema Maua Sama, Ben Pol pamoja na Diamond ni miongoni mwa wasanii anaotamani kufanya nao kazi.
“Sijawahi kufanya kazi na Maua Sama, lakini natamani kufanya kazi na Maua Sama kutokana na ubora wa sauti yake. Kwahiyo Maua Sama ni mmoja kati ya wasanii ambao naimani naye. Pia natamani kufanya kazi na Ben Pol, sijawahi kufanya kazi na Ben Pol.,” alisema Hermy B
Aliongeza, “Pia natamani kufanya kazi na Diamond kutokana na sauti yake na jinsi ambavyo anavyoweza kuitwist. Halafu one thing ni kwamba Diamond ana element ambayo watu wengi hawaijui, Diamond ni rapper.”
0 comments:
Post a Comment