Lady Jaydee kula na mashabiki wake





Mkali wa wimbo wa ‘Ndi ndi ndi’, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, ameonyesha kuwateka mashabiki wake kwa kuchagua video tatu nzuri wanazomtumia kisha anakwenda kula nao chakula cha jioni na kuwa nao katika matukio yake makubwa ya kimuziki.

Katika maelezo yake aliyoweka katika ukurasa wake wa facebook, Jay Dee aliandika kwamba waliomtumia video wakiwa wanaimba wimbo wa ‘Ndi ndi ndi’ atachagua majina matatu ya walioburudisha vema zaidi kisha atawataja siku zijazo kwa ajili ya chakula hicho.

“Nitachagua ‘Clips 3’ bora zilizokonga na kusuuza watu wengi na watatu hao nitafanya mchakato wa kula nao japo ‘dinner’ pamoja na ‘ku-hang’ nao siku yoyote nikiwa na ‘event’ kubwa, majina nitataja baadaye kidogo,’’ aliandika Jay Dee.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment