Taifa Stars ya Tanzania inashuka uwanjani kuikabili Chad



Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itashuka uwanjani hapo kesho, huko nchi Chad katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017.



Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 11 kwa saa za nyumbani Afrika Mashariki.

Taifa Stars, imefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo katika uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya ulipo katika jiji la D’jamena.

Kocha anayekinoa kikosi hicho Charles Boniface Mkwasa amesema anashukuru vijana wake hakuna majeruhi na wote wameweza kufanya mazoezi aliyoyapangilia.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment