Adele (27) ametangazwa kuwa ni msanii wa kike tajiri kwa Uingereza na Ireland ambaye hajawahi kutokea.
Gazeti la Sunday Times limetoa ripoti hiyo kuwa kwa sasa Adele ana utajiri wa paundi milioni 85 ukilinganisha na mwaka jana ambapo alikuwa na utajiri wa paundi milioni hamsini.
Kwa sasa Adele anashika nafasi ya 30 kwa wasanii matajiri kwa UK na Ireland akipanda tofauti na mwaka jana aliposhika nafasi ya 43. Adele amewazidi wasanii wengine kama Sir Cliff Richard, Gary Barlow and Kylie Minogue.
Hii ni top 10 ya wasanii matajiri wanaoongoza kwa Uingereza na Ireland
1. Sir Paul McCartney and Nancy Shevell £760m
2. Lord Lloyd-Webber £715m
3. U2 £500m
4. Sir Elton John £280m
5. Sir Mick Jagger £235m
6. Olivia and Dhani Harrison (wife and son of the late George Harrison) £220m
7. Keith Richards £220m
8. Ringo Starr £200m
9. Michael Flatley £198m
10. Sting £185m
0 comments:
Post a Comment