Afande adai 20 Percent anateswa na tuzo 5 za Kili


Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro Afande Sele, amesema 20 Percent anateswa na tuzo tano za Kili Music Awards alizochukua mwaka 2011 ndio maana kila akitoa wimbo unashindwa kufanya vizuri.



Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Alhamisi hii, Afande amesema 20 Percent toka achukue tuzo, ameshindwa kabisa kurudi kwenye muziki.

“Ni kweli zinamtesa mimi naamini hivyo. Kwa hiyo nathubutu kusema zimemtesa na zinaendelea kumtesa,” alisema Afande.

20 Percent ameshajaribu kutoa nyimbo kadhaa lakini zimeshindwa kuteka hisia za mashabiki wake kama nyimbo zake za zamani.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment