Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya ‘TUMA’ waja kivingine ili kutetea haki za wasanii


Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya, yaani Tanzania Urban Music Association (TUMA), kimezindua kamati tano ambazo zitakisaidia chama hicho kuwahudumia wanachama wake ipasavyo.


Mratibu Mkuu wa TUMA, Samuel A. Mbwana aka Braton (Kulia) akiwa na Bagdad mmoja kati ya wanakamati waliyotajwa

Kamati hizo ni, Kamati ya nidhamu na maadili ya Chama inasimamiwa na Stara Thomas na Moses Papa, Kamati ya Burudani na Matukio inasimamiwa na Witness na Adiliwa, Kamati ya Mipango, fedha na Uchumi inasimamiwa na Lucc, Mwana FA na Dan Msimamo, Kamati ya Habari na Mawasiliano inasimamiwa na HK na Baghdad na Kamati ya mwisho ni Kamati ya Ushirikiano wa Kitaifa na Kimataifa ambayo inasimamiwa na Wakazi pamoja na K-Eisher.

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa TUMA, Samuel A. Mbwana aka Braton, amesema wao kama TUMA wameamua kuja kivingine ili kuongeza kasi ya kutatua changamoto mbalimbali za wasanii.

“Huu ni wakati wa wasanii kuungana, kujiunga na chama cha TUMA ili tuweze kusaidiwa kwa pamoja, kwa sababu hata rais alishasema hawezi kumsaidia msanii mmoja mmoja, tuungane ili tusaidiwe kwa pamoja kama chama. Kwa hizi kamati kwa ujumla zitakuwa zinafanya kazi mbalimbali kama ambavyo zenyewe zinajihainisha,” alisema Braton.

Aliongeza, “Kwa hivyo katika kuboresha ufanisi na utendaji wa chama, hii leo chama kinapenda kutangaza kamati ya utendaji ya Chama ili kusimamia, kubuni na kutekeleza mipango ya chama a kwa faida ya wanachama”,

Braton akionyesha kadi za wanachama

Pia Braton alisema chama kimedhamiria kuwa chama bora kati ya vyama vinavyounda shirikisho la muziki Tanzania japo kuwa kina wanachama wachache tofauti na wingi wa wasanii.

Braton alisema TUMA kwa sasa kina wanachama zaidi ya 60, na wameandaa utaratibu mzuri wa kuwagaia kadi za uanachama ili kukitangaza chama na nchi kwa ujumla.

Hata hivyo, Baghdad ndiye mwanakamati pekee aliyejitokeza katika mkutano huo wa waandishi wa habari.

Credit Bongo5
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment