Kuondoka kwa KR ndani ya Wanaume Halisi ndiyo mwisho wa kazi za Nature?



KR Mullah amesema kuwa inawezekana Juma Nature hajapendezewa na yeye kujiunga na Radar Entertainment.



Siku kadhaa baada ya KR kuhama Wanaume Halisi na kuhamia Radar Ent, Nature alimtahadharisha kuwa makini nao wasije wakamuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, KR alisema, ‘Nature anaona kazi zake zitalega lega baada ya mimi kuhamia Radar Entertainment’.

“Nilikuwepo ndani ya kundi la Wanaume Halisi, sasa labda anavyoona mi nipo huku ina maana yeye anaona kazi zake tena zitakuwa zinalega lega. Labda hakupendezewa mimi kwenda kufanya kazi na yule mtu na kwamba yeye alitegemea mimi niendelee kufanya kazi naye. Siku zote wanasema watu ni kubadilisha mazingira, kubadilisha sanaa, kikubwa aniache nitingishe tu aniache,” aliongezea KR.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment