Mahrez ashinda tuzo ya mchezaji bora Uingereza



Usiku wa April 24 mshambuliaji wa Leicester City Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya chama cha wachezaji soka ya kulipwa Uingereza (PFA) Mahrez ni raia wa Algeria anakuwa mchazaji wa kwanza Afrika kushinda tuzo hiyo.



Mahrez amefunga mabao 17 na kusaidia katika ufungaji wa mengine 11 katika mechi 34 za ligi alizochezea Leicester na kuwasaidia sana kukaribia kushinda taji la ligi.

Riyad Mahrez ametangazwa kushinda tuzo hiyo mbele ya wachezaji kama Mesut Ozil wa Arsenal, Jamie Vardy wa Leicester City, Harry Kane wa Spurs, N’golo Kante wa Leicester City, Dimitri Payet wa West Ham United, PFA ni tuzo za wachezaji bora wa kulipwa.

Wachezaji soka ya kulipwa Uingereza ndio hupiga kura kuamua mshindi.

Kiungo wa kati Tottenham Dele Alli, 20, ndiye aliyeshinda tuzo ya PFA ya mchezaji chipukizi wa mwaka naye mshambuliaji Izzy Christiansen akashinda tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka.

Mahrez alipokezwa tuzo katika hoteli ya Grosvenor, London Jumapili saa chache kabla ya kufunga bao na kusaidia Leicester kulaza Swansea City 4-0.
Leicester wanahitaji kutwaa alama tano kutoka kwa mechi tatu walizosalia nazo ili kushinda ligi.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment