Nikujitia unyonge kulalamika nyimbo zako hazichezwi kwenye radio – Sugu



Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema huu sio wakati wa wasanii kuendelea kulalamika kwamba nyimbo zao hazichezwi kwenye vituo vya radio.

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Sugu amesema kutanuka kwa teknolojia kumewapa wasanii uwanja mpana wa kusambaza kazi zao bila kutegemea kituo kimoja cha radio.

“Unajua zamani kulikuwa kuna vituo vichache vya radio alafu kati ya hivyo kimoja ndo kimekamata zaidi, lakini sasa hivi radio zipo kila mahali, mitandao ya kijamii. Kwa hiyo kuna media nyingi sana, yaani kuna namna nyingi za kufikisha muziki wako kwa jamii. Kwa hiyo ni kujitia unyongo wewe mwenyewe kung’ang’ana kwamba fulani hapigi nyimbo zako,” alisema Sugu.

Aliongeza, “Kwa mfano mimi sasa hivi, ukiniuliza sijui vipi nani atapigia wimbo nani hapigi, nitajibu mimi sijali nani hapigi nani anapiga kwa sababu tutasambaziana na washikaji kwenye mitandao. Kwa hiyo wasanii ambao bado wanazilalamikia radio wabadili mitazamo yao ya kibiashara, dunia haipo huko sasa hivi. Kwanza wasanii ndio wana nguvu ya kutokumpa nguvu mmiliki wa radio, kwa mfano kama hilo tatizo lipo watu waungane sasa, waseme na sisi kuanzia leo, ni marufuku kucheza nyimbo zetu, hiyo radio itaendeshwajwe?, kwa hiyo huu sio wakati wa kulalamika,”

Credit bongo5
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment