Ommy Dimpoz aingia kwenye biashara hii


Zamani tuliamini kuwa kilimo hufanywa na watu wanaoishi vijijini tu. Mambo yamebadilika na kwasababu sasa hivi hakichukuliwi kama kilimo peke yake, bali biashara ya kilimo na leo vijana wengi wa mjini wamejiingiza huko sababu kinalipa.




Wakati ambapo unadhani kuwa Ommy Dimpoz yupo kimya kimuziki, basi anapenda kukufahamisha kuwa naye ni miongoni mwa vijana wa mjini walioingia kwenye biashara hiyo.

Alipost picha Instagram akiwa kwenye shamba lake na kuweka emoji za matunda, ikiashiria kuwa huenda atafanya kilimo cha aina hiyo kwa sasa.

Ni jambo zuri kwa vijana kuingia kwenye kilimo hasa kwakuwa tangu zamani inafahamika kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa na katika zile fursa 10 alizotaja Ruge Mutahaba, hiyo ni fursa ya kwanza. Heko Dimpoz.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment