Polisi wanasa saa ya dola milioni moja Nigeria




Polisi wanasa saa ya dola milioni moja Nigeria

Polisi wa kupambana na ufisadi nchini Nigeria, wamenasa saa ya thamani ya takriban dola milioni moja kutoka kwa nyumba ya waziri wa zamani wa mafuta anayechunguzwa kwa ufisadi.

Saa hiyo ya kipekee ni moja tu kati ya makumi ya mapambo ya dhahabu almasi na fedha zilizonaswa katika operesheni hiyo ya kuvizia katika nyumba ya aliyekuwa waziri wa mafuta wa Nigeria katika utawala uliopita bi Diezani Madueke.

Diezani Alison Madueke- waziri wa zamani wa mafuta wa Nigeria

Shirika la kupambana dhidi ya ufisadi la Nigeria (Economic and Financial Crimes Commission) limeithibitishia BBC kuwa bi Madueke anachunguzwa kufuatia madai ya ufisadi.

Mabilioni ye fedha zilitoweka katika wizara hiyo akiwa mamlakani.


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameapa kutokomeza ufisadi

Fedha hizo zilikuwa sehemu ya mapato yanayotokana na mauzo ya mafuta katika soko la kimataifa.

Mwaka uliopita bi Madueke alikamatwa na kuhojiwa na maafisa wa upelelezi wa Uingereza lakini akaachiwa kwa dhamana.
Image copyrightAFP GettyImage captionMabilioni ye fedha zilitoweka katika wizara hiyo akiwa mamlakani.

Rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alichaguliwa kwa nia ya kumaliza kabisa ufisadi uliokuwa umekithiri nchini humo.

Rais Muhammadu ameahidi kutokomeza kabisa ufisadi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment