Staa wa muziki nchini, Diamond Platnumz na wasanii wa Afrika Kusini, Mafilizolo, wametua bungeni Dodoma Alhamisi hii kusikiliza randama ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Kutoka kulia, msanii wa kundi la Mafikizolo, Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye, Diamond Platnumz, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba, wakiwa nje ya bunge.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Diamond, alipost picha na kuandika:
Dakika chache zilizopita nikiwa na Mafikizolo tukiwa na Mh Waziri @JMakamba2015 na #NapeNauye Bungeni Dodoma….. #ColorsOfAfrica Cc @theoMafikizolo @nhlanhla_nciza ….Suit by my Favorite suit Designer @Speshoz
0 comments:
Post a Comment