Gareth Bale amemsifia mocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane kwa kuwafanya wajiamini hadi kushinda ligi ya mabingwa wa Ulaya wikiendi iliyomalizika.
Ushindi huo wa 11 wa Real wa kombe la Ulaya ulikuja kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Atletico Madrid jijini Milan Jumamosi baada ya kutoka sare ya 1-1. Bale, aliyefunga mkwaju wa kwanza ammemwagia sifa mocha huyo wa Ufaransa aliyeziba nafasi ya Rafa Benitez aliyefukuzwa January.
Bale alisema: “Amekuja na amekuwa mtu mzuri kwa kila mmoja. Ametufanya tujiamini, ule uhuru wa kucheza. Ameiunganisha timu. Kwahiyo sote tunacheza kwa kufurahia tukiwa chino take na imeonesha usiku hii kile tulichofanya.”
Huo ni ubingwa wa pili kwa Bale akiwa na Real baada ya ushindi wa 4-1 baada ya muda wa nyongeza na hao hao Atletico kwenye fainali iliyofanyika jijini Lisbon mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment