Mashabiki wa Justin Bieber waandamana Argentina kupinga kuzuiwa kwa show yake



Mamia ya mashabiki wa Justin Bieber
“Beliebers” wameandamana kwenye mji mkuu wa Argentina kuzitaka mamlaka za nchini humo kumruhusu msanii huyo wa Canada atumbuize kwenye nchi hiyo ya Amerika Kusini.



Justin Bieber alitangaza Jumatatu iliyopita kwenye Twitter kuwa angependa kuipeleka ziara yake ya Purpose nchini hump hadi pale masharti ya kisheria yaliyowekwa yakibadilishwa.

Muimbaji huyo aliwahi kushtakiwa kwa kuwatuma walinzi wake waende kumshambulia mpiga picha nje ya klabu ya usiku ya Buenos Aires alikuwa ziarani nchini humo mwaka 2013.

Mamia ya mashabiki hao waliandamana katikati ya Buenos Aires wakiwa na mabango yaliyosomeka
“Argentina Needs Justin” na “Right To Music.”

Mmoja wa waandamaji alisema kama jaji wa kesi hiyo ana moyo atamruhusu Bieber atumbuize nchini humo.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment