Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Mchizi Mox anajipanga ili kuachia wimbo wake mpya ‘Oya Oya’ ambao utakuwa maalum kwa ajili ya watafutaji.
Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Mchizi Mox amesema wimbo huo utawafanya vijana kuongeza juhudi katika kusaka mkwanja.
“Sasa hivi na project mpya inaitwa Oya Oya, ni ngoma ambayo itakuwa inahamasisha sana watu kufanya kazi kwa juhudi, yaani ni meseji fulani ambayo inawafanya waangaikaji waendelee kutafuta, kwa hiyo ni kazi ambayo itasumbua mtaani,” alisema Mox
Mox amesema kuwa kwa sasa atakuwa anatoka kazi mara kwa mara tofauti na wakati wa nyuma ambao alikuwa anakaa muda mrefu bila kutoa ngoma.
0 comments:
Post a Comment