Prezzo akanusha kubwia unga


Rapper wa Kenya, Prezzo amekanusha kutumia madawa ya kulevya kama ambavyo kumekuwepo na minong’ono hiyo kwa muda mrefu.



Akiongea na Clouds E ya Clouds FM, Prezzo alisema hajihusishi na madawa ya kulevya na kukonda kwake kumetokana na yeye mwenyewe kutaka awe hivyo.

Prezzo amekuja Tanzania ambapo amefanya collabo na hitmaker wa ‘Siwezi’ Barakah Da Prince katika studio za Fish Crub chini ya producer Lamar. Amesafiri na producer na mshkaji wake, Sappy.

Akiongea na huku akionesha dhahiri akiwa amekula chupa mbili tatu za ulabu (kitu ambacho anadai ni uchovu na usingizi kutokana na kuwa busy kwenye tour), Prezzo alisema kuwa binadamu watamsema vyovyote atakavyokuwa awe mwembamba au mnene.

Siku hivi karibuni rapper maarufu kwa pamba, ameonekana kutulia zaidi huku akimtambulisha mpenzi wake Michelle aliyekuja naye pia Dar.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment