Rais Magufuli Mgeni Rasmi Mkutano Wa CRB


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Nchini (CRB) leo tarehe 26 Mei, 2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.


Mkutano huo wa mwaka wa mashauriano na wadau wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya Makandarasi na wadau wa Sekta ya Ujenzi wapatao 1000 na utafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 26 Mei, 2016 hadi tarehe 27 Mei 20l6.


Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Juhudi za Makusudi za Kukuza Uwezo wa Makandarasi Wazalendo kwa Maendeleo Endelevu ya Kiuchumi; Changamoto na Mustakabali Wake’.


Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau wa Bodi ya Usajili Makandarasi na Sekta ya Ujenzi ili kujadili changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kuwajengea uwezo Makandarasi Wazalendo.


Imetolewa;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Source Mpekuzi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment