TID asema hana taarifa kama Billnas ameondoka Rada Entertainment


Baada ya hivi karibuni rappa Billnass kutangaza kuachana na label yake ya zamani ‘Rada Entertainment’ na kujiunga na ‘LFLG’, Mkurugenzi wa Rada Entertainment, TID ‘Mnyama’ amesema hana taarifa rasmi kwamba Billnass hayupo Rada Entertainment.



Akizungumza na Bongo5 Jumapili hii, TID amesema hana taarifa ya kwamba msanii wake, Billnass amesaini label mpya.

“Rada tupo safi sana, Billnass yupo, na mimi sina taarifa kama Billnass ameondoka Rada, bado mimi najua ni msanii wa Rada,” alisema TID.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Confidence’, amewataka mashabiki wa muziki wake kusubiria kazi zake binafsi pamoja naza Rada.

Credit bongo5

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment