Billnass asema Mr Blue ndiye msanii anayeongoza kwa kuigwa flow kuliko msanii yeyote


Mkali wa wimbo ‘Chafu Pozi’ Billnass amefunguka kwa kusema kuwa Mr Blue ndiye msanii pekee anayeongoza kwa kuigwa flow kuliko msanii yeyote nchini.


Rapper huyo ambaye mara nyingi flow zake zimekuwa zikifananishwa naza rapper Godzilla, amesema yeye haoni ambapo anafanana na rapper huyo mwenye makazi yake Salasala jijini Dar es salaam.

“Hapana mimi sirap kama yeye (Godzilla) na sioni sehemu ambayo nafanana kama yeye, na mtu kufanana na mtu haiwezi kuwa tatizo,” Billnass aliimbia Global TV.

Aliongeza, “Mtu ambaye anaongoza kwa kuchukuliwa sana flow zake hapa Tanzania ni Mr Blue, kwa sababu wametokea sana wasanii wengi ambao wanafanana na Blue lakini sijawahi kusikia hicho kitu akikizungumzia au kulalamika na bado Blue anabaki kuwa Blue. Kwa hiyo kama kulalamika na ningekuwa nimechukua style yake ingekuwa ni heshima kwake kwa sababu kuna mtu anafanya kama yeye na ingembakiza mara dufu,”




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment