Msanii wa muziki, Christian Bella akishirikiana na Linex Sunday, Jumatatu hii wanatarajia kuachia wimbo wao wa pamoja uitwao ‘Hewala’.
Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Bella amesema kazi hiyo itakuwa tofauti na kazi zake za nyumba ambazo amewahi kufanya.
“Tulichokifanya nyuma na hiki tulichokifanya sasa hakiwezi kuwa sawa sawa, kwa hiyo mashabiki wataona vitu tofauti ambazo hatujawahi vifanya, mbwembwe na mawazo mapya,” alisema Bella.
Aliongeza, “Kwenye kazi hii mpya, filling mpya, melody mpya, kila kitu ni kipya hata video. Tunaanza kutoa kwanza audio kwa sababu tumeamini ngoma ni kali, baada ya audio tutatengeneza video soon kwa sababu hatuwezi kukaa muda mrefu bila kuachia video,”
Muimbaji huyo amesema wimbo huo utatoka siku ya Jumatatu.
Credit Bongo5
0 comments:
Post a Comment