Hanscana asema 80% ya video za muziki za TZ anashoot yeye, awataka wenzake kukaza



Mtayarishaji wa video za muziki nchini kutoka Wanene Films, Hanscana amesema tayari ameshafanikiwa kuliteka soko la video za muziki nchini ambapo amedai karibu 80% ya video za muziki Tanzania anashoot yeye.



Hanscana

Muongozaji huyo ambaye pia alikuwa mshindi wa Tuzo za Watu 2015 kwenye kipengele cha muongozaji wa video za muziki anayependwa, ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo inamfanya kuwa busy kwa muda mrefu.

“Kwa sasa nafanya kazi kubwa sana, kwa sababu karibu 80% ya video za Tanzania nashoot mimi, na 20% zinaenda kwa wengine, na 10% South Africa,” alisema Hanscan. “Kwa hiyo nakuwa busy sana, madirector wengine wakikaza zaidi tutasaidiana,”

Video ambazo ameongoza hivi karibini ni ‘Bayoyo’ ya AbduKiba, ‘Arosto’ ya G.Nako & Chin Bees & Nikki wa Pili, ‘Freedom’ ya Sugu, ‘My Life’ ya Dogo Janja, ‘Fundi’ ya Mh. Temba pamoja na nyingine nyingi.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment