Jay Moe asema hajarudi kwenye game ili ashindane na wanaofanya vizuri


Rapper Jay Moe amesema kuwa hajarudi kwenye game la muziki ili kushindana na wasanii wanaofanya vizuri, bali amerudi ili kukata kiu ya muziki kwa mashabiki wake ambao walikuwa wanamsubiria kwa muda mrefu.


Akiongea katika kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television Ijumaa hii, Jay Moe amesema yeye anaamini bado nafasi yake kwenye muziki ipo.

“Mimi sijarudi kwenye game ili nishindane na waliopo, nimekuja kutoa burudani kwa mashabiki wangu ambao walinimis kwa muda mrefu, pia nikikutana na hao wasanii ambao mnawasema wananiambia Jay Moe bado game linakuhitaji, kwa hiyo mimi narudi kwenye game ili kutoa burudani kwa mashabiki wetu, kwa sababu mimi naamini mashabiki wa Joh Makini na wasanii wengine ndio wale wale mashabiki wa Jay Moe,” alisema Jay Moe.

Moe amewaka mashabiki wa muziki wake kusupport wimbo wake mpya uitwao ‘Pesa Ya Madafu’.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment