Nedy Music adai kuwa hakuna chipukizi anayemsumbua kimuziki





Msanii chipukizi anayekuja kwa kasi katika tasnia ya Bongo Fleva, Sai Seif Ally ‘Nedy’, amefunguka kuwa hakuna chipukizi anayemuumiza kichwa.

Nedy aliliambia gazeti la Mtanzania kwamba, anatambua kila msanii hutoka kwa kasi kubwa na hukubalika kwa mashabiki wake lakini kwake hakuna anayeweza kumtisha kisanii.

“Ninaiamini kazi yangu hivyo hakuna msanii atakayeniumiza kichwa katika tasnia yetu ya muziki,” alisema.

Msanii huyo aliye chini ya lebo ya ‘PKP’ kwa sasa anatamba na video yake inayojulikana ‘Usiende Mbali’ alioshirikiana na Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment