Demba Ba asema haya kuhusu kucheza soka baada ya kuvunjika Mguu
Mshambulaiji wa kimataifa wa Senegal na klabu ya Shanghai Shenhua Demba Ba, ameeleza mustakabali wa soka lake baada ya kuvunjika mguu akiwa katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini China mwishoni mwa juma lililopita.
Baada ya mechi hiyo, mkufunzi wa mshambuliaji huyo Gregorio Manzano alisema jeraha hilo “huenda likafikisha kikomo uchezaji wake”.
Lakini Ba amenukuliwa na radio ya China ya Monte Carlo akiwa hospitali kuwa hatazamii kustaafu karibuni kutokana na kuvunjika sehemu mbaya ya mguu wake wa kushoto, pamoja na hayo Demba Ba amesema hajafanyiwa upasuaji kamili kutokana na yeye mwenyewe kutaka kwenda Ulaya kutibiwa.
“Hili ni jeraha baya sana lakini ninaweza kujikwamua. Sitafikisha kikomo uchezaji wangu hapa, hilo nina uhakika nalo,” amesema Ba, mwenye umri wa miaka 31.
“Msimu hapa unamalizika Novemba na kuanza Machi. Nitajizatiti kurejea kwa wakati kwa msimu utakaofuata.” alisema Ba
Demba Ba aliwahi kuzicheza vilabu vya West Ham, Newcastle na Chelsea katika Ligi ya Premia.
Alijiunga na Shenhua kutoka klabu ya Besiktas ya Uturuki, akinunuliwa takriban pauni 12 milioni mwezi Julai mwaka jana.
Kwa sasa, ndiye mfungaji mabao bora Ligi Kuu ya Uchina akiwa na magoli 14 kutoka mechi 18.
0 comments:
Post a Comment